Godzila kuacha muziki kwa muda
Mwanamuziki toka pande za Salasala, The King of Salasala, Godzila, hatopanda jukwaani tena mpaka apone kidonda kilichoshonwa nyuzi.
Godzila alisema alipata  ajali wakati akitoka Mikocheni kwenda Studio, na punde tu walipofika njiani Coaster moja, ilikuja na kuwagonga kwa nyuma kiasi cha kujigonga na kuchanika sehemu ya mdomoni.
Amesema baada ya tukio hilo ilimbidi afike hospitali na kushonwa nyuzi mbili, ambazo hadi sasa bado anafuatilia matibabu.
Hivyo amesema hatuweza kupanda jukwaani mpaka hali yake itakapotengemaa na kuwa sawia ndipo ataingia tena mzigoni kwa ajili ya burudani zaidi.
Leave a Reply
Sorry, but you must be logged in to post a comment.




1 Comment
by peter
On January 6, 2012
no comment to you guy welcome a town we ni mkali sna ila take care sna coz wanaokuchukia uwajui wapo karibu yako sana tht it iz